NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 93

1 Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.

2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele.

3 Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.

4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu.

5 Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0