NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 87

1 Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:

4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”

6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”

7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0