NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 82

1 Zaburi ya Asafu. Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:

2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

3 Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa.

4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika.

6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’

7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”

8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0