NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 67

1 Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,

2 ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote.

3 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

4 Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia.

5 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

6 Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

7 Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0