NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 23

1 Zaburi ya Daudi. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

2 Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza,

3 hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4 Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.

5 Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika.

6 Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0