NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 149

1 Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

2 Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

3 Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

4 Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.

5 Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.

6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,

7 ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa,

8 wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma,

9 ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0