🔍 Tafuta katika BibliaZaburi 134
1 Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.
2 Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana.
3 Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0