NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 133

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.

3 Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0