NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 130

1 Wimbo wa kwenda juu. Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.

3 Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?

4 Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.

5 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

6 Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.

7 Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.

8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0