NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 13

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini?

2 Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini?

3 Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.

4 Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

6 Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0