NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 129

1 Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:

2 wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.

3 Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.

4 Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.

5 Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.

6 Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8 Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0