NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 128

1 Wimbo wa kwenda juu. Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake.

2 Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.

4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.

5 Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,

6 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0