NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 126

1 Wimbo wa kwenda juu. Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto.

2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Bwana amewatendea mambo makuu.”

3 Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.

4 Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu.

5 Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.

6 Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0