NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 124

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa:

2 kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia,

3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai,

4 mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika,

5 maji yaendayo kasi yangalituchukua.

6 Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

7 Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka.

8 Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0