NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 122

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.”

2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.

3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.

4 Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli.

5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.

7 Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.”

8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

9 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0