NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 121

1 Wimbo wa kwenda juu. Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi?

2 Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.

3 Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,

4 hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.

5 Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

6 jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku.

7 Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako,

8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0