NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 120

1 Wimbo wa kwenda juu. Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu.

2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu.

3 Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?

4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.

5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!

6 Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.

7 Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0