NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 117

1 Msifuni Bwana, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote.

2 Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa Bwana unadumu milele. Msifuni Bwana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0