NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Zaburi 114

1 Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,

2 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake.

3 Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma,

4 milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo.

5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,

6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo?

7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo,

8 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0