NENO
🔍 Tafuta katika Biblia

Ayubu 25

1 Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

2 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

5 Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,

6 sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Kiswahili Contemporary Version). Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. CC BY-SA 4.0